Gloria Ntazola asimulia hali halisi baada ya mzozo na afisa wa kanjo

Kulingana na yeye,afisa huyo wa kanjo aliingia ndani ya gari lake kwa lazima akitaka kumkamata kwa sababu ya kuegeza gari

Muhtasari

• Katika mahojiano ya moja kwa moja na Radio Jambo,Ntazola amesema alifikia uamuzi huo baada ya maafisa hao kumvamia kwa kuegeza gari lake,baada maafisa hao kuvamia wachuzi wengine.

• "Nilimkataza asiingie kwa gari langu lakini akaingia kwa lazima,nilishikwa na hasira na hivyo nikataka kumpa funzo,kwa sababu hii si mara ya kwanza yeye kunifanyia hivyo,"

Gloria Ntazola
Gloria Ntazola
Image: Instagram

Muundaji maudhui na mwanabiashara Ntazola Gloria amesimulia hali halisi aliyokumbana nayo wakati mzozo kati yake na afisa wa kanjo ulitokea hapo awali.

Katika mahojiano ya moja kwa moja na Radio Jambo,Ntazola amesema alifikia uamuzi huo baada ya maafisa hao kumvamia kwa kuegeza gari lake,baada maafisa hao kuvamia wachuzi wengine.

Gloria,amesema wazi kuwa afisa huyo alikuwa na mazoea kwani hii haikuwa mara yake ya kwanza kumfanyia tendo hilo la kuitisha hongo kila wakati akiegeza gari lake.

Kulingana na yeye,afisa huyo wa kanjo aliingia ndani ya gari lake kwa laziam akitaka kumkamata kwa sababu ya kuegeza gari bila kulipia akajaribu kumkanya ila akasisitiza.

"Nilimkataza asiingie kwa gari langu lakini akaingia kwa lazima,nilishikwa na hasira na hivyo nikataka kumpa funzo,kwa sababu hii si mara ya kwanza yeye kunifanyia hivyo,"alisema.

Mwanabiashara huyo anayeendesha biashara ya vipodozi,amesimulia jinsi maafisa hawa wa kanjo wanaghadhabisha watu wakati wanapofanya shughuli za ushuru jijini.

Vilele amedhibitisha kuwa hasira yake ilijumuishwa pamoja na taarifa ya hapo awali mbapo maafisa hao walikuwa wamewadhulumu wachuuzi katika jiji na hivyo kupelekea kumuadhibu afisa huyo kwa kumpeleka safari ambayao hakuwa ametarajia.

Ntazola anasema alipokea simu kutoka kwa polisi ya kumtaka kuandikisha tarifa,na kusema kuwa kwa sasa polisi wanaendesha uchunguzi ili kubaini  yupi aliyekuwa na makos.

Aidha ameoma msamaha wake kwa wakenya na mashabiki wake kwa jumla kwa matusi aliyotamka akiwa hewani akisema kuwa yalichangiwa na kupandwa mori.

Ntazola sasa amesema yuko tayari kuwa na mazungumzo na afisa huyo ili kuomba msamaha ikiwa atapatikana na makosa baada ya uchunguzi kumalizika.