Gloria Ntazola,muunda maudhui aliyezozana na afisa wa kanjo hapo awali amejitokeza wazi na kusema kuwa vitendo vyake vilipata ukusoaji mwingi.
Akizungumza na Radio jambo,Ntazola amesema kuwa watu wa familia pamoja na baadhi ya mashabiki walipata kukosoa vitendo vyake vilivyohusisha mzozo kati yake na afisa wa kanjo uliotokea hivi majuzi.
"Nilipata ukosoaji wa kila aina kutoka kwa wanafamilia hasa mama yangu amabye ni pasta,mashabiki na watu wengine wa karibu,"alisema.
Hata hivyo amesisitiza kusema kuwa alichokifanya kulingana na yeye ni sawa akidai maafisa hao wana tabia ya kupitiliza kwa jinsi wanavyo kabidhiana na wanabiashara jijini.
"Kwangu mimi nilifanya kitu sawa,watanikooa ndio lakini sijutii maana nilikuwa nataka kutoa funzo," alisisitiza.
Gloria anasema kuwa mama yake ambaye alimtaja kuwa pasta,alidhadhabishw na vitendo hivyo hasa vya kutaja matamshi ya matusi huku umma ukimtazama,jambo ambalo aliema alilichukulia kama la kushusha hadhi yake.
Baadhi ya mahabiki walimpongeza,wakidai kuwa Gloria ni mwanamke bomba kwani alichukua jukumu la kuweka wazi tabia ya maafisa wa kanjo amabyo imekolea wazi.
Ntazola amemiminiwa sifa huku wengi wakisema inatakiwa watu kuchukua msimamo kama wa wake ili kukomesha ufisadi nchini, jambo ambalo wanadai limeudisha uchumi wa taifa nyuma.
Ntazola sasa amesema kuwa anasubiri mustakabali wa uchunguzi unaoendelea ili kubini azma ya kesi hiyo ambayo kwa sasa iko mikononi mwa polisi.
Hapo awali,Ntazola alilalamikia akaunti yake ya TikTok kufungwa baada ya mzozo huo kutokea,jambo ambalo anahisi,lilisababishwa na kutumia lugha chafuwakati akimrekodi afisa huyo wa kanjo.
Hata hivyo aliweza kufungua akunti mpya ambayo sasa anasema imepata umaarufu tena akieleza kushangazwa jinsi mashabiki wake waliweza kujibu kwa kumfuata katika aknaunti hiyo mpya.
“Akaunti yangu ilizama nafikiri ni kwa vile nilitumia lugha ya matusi dhidi ya kanjo, lakini baada ya kuwaambia watu nimeanzisha akaunti mpya nilishangazwa sana kwa jinsi walinifuata kwa haraka na kwa wingi, kwa sasa niko na wafuasi Zaidi ya elfu 50,” alisema kwa furaha.