Bensoul azungumzia sababu ya kuvunjika kwa mahusiano yake, ushirikiano na mzazi mwenzake

Bensol alibainisha kuwa yeye na Bi Gathoni wanafurahia hali yao mpya baada ya kutengana

Muhtasari

•“Ilifika mahali hakuna mapenzi. Sisi sote tuna furaha sasa. Hakuna haja ya kulazimisha kitu mhangaike baadaye,” Bensol alisema.

• Bensol alibainisha kuwa yeye na mzazi mwenzake wamekuwa wakishirikiana vyema katika malezi ya binti yao.

katika studio za Radio Jambo.
Bensol na mtangazaji Massawe Japanni katika studio za Radio Jambo.
Image: RADIO JAMBO

Msanii wa Sol Generation Benson Mutua Muia almaarufu Bensoul amefichua kwamba mahusiano yake na mpenzi wake wa muda mrefu Noni Gathoni yalifikia kikomo baada ya mapenzi kuisha.

Akizungumza wakati wa mahojiano na mtangazaji Massawe Japanni kwenye Radio Jambo, Bensoul alibainisha kuwa yeye na Bi Gathoni wanafurahia hali yao mpya baada ya kutengana.

“Ilifika mahali hakuna mapenzi. Sisi sote tuna furaha sasa. Hakuna haja ya kulazimisha kitu mhangaike baadaye,” Bensoul alisema.

Mwimbaji huyo alisema kuwa ameridhika na maisha ya ukapera na akabainisha kuwa sasa anaweza kuzingatia muziki wake na majukumu ya uzazi.

“Mahusiano yaliisha tu. Unajua mapenzi huisha. Nina raha vile niko single. Kazi yangu sasa ni muziki wangu na kulea binti yangu,” alisema.

Bensoul alifichua kuwa yeye ndiye aliyemaliza mambo na mpenzi huyo wake wa zamani na kuweka wazi kuwa hatua ya kuachana haikuwa na athari yoyote kwake.

“Kuachana kuliniongeza nguvu ya kufanya zaidi. Hakukuniathiri. Mimi ndiye nilimaliza mambo,” alisema.

Mwanamuziki huyo alithibitisha kusambaratika kwa mahusiano yake na Noni Gathoni mapema mwaka huu baada ya kuwa kwenye uhusiano na mshawishi huyo wa mitandao ya kijamii kwa muda mrefu.

"Niko kama Harmonize I am single si mingle but I'm single.." Bensoul alisema kwenye mahojiano na Mungai Eve mnamo Aprili.

Licha ya kuchumbiana kwa muda mrefu, Bensoul na Gathoni hawakuwahi kupata mtoto pamoja. Msanii huyo hata hivyo ana mtoto wa kike na mwanamke anayejulikana kama Tiffany Muikamba.

Akizungumza na Massawe Japanni Jumanne, baba wa mtoto mmoja alibainisha kuwa yeye na mzazi mwenzake wamekuwa wakishirikiana vyema katika malezi ya binti yao.

“Mtoto ako na mama yake lakini namuona siku nyingi. Tuko na maelewano mazuri,” alisema.

Bensoul pia aliweka wazi kuwa katika siku za usoni yuko tayari kujaribu mahusiano tena na mwanamke kutoka mahali popote ulimwenguni.

“Mapenzi hujui yatatoka wapi. Nikipendwa na mjerumani ni sawa. Nikipendwa na Mjamaica ni sawa,” alisema.