Rapa Vera Sidika afichua jinsi mumewe Brown Mauzo alivyopiga jeki azma yake ya muziki

Mwanasoshalaiti huyo aliweka wazi kuwa Mauzo ni shabiki wake mkubwa sana.

Muhtasari

•Katika mahojiano na Massawe Japanni, rapa huyo mpya zaidi mjini alifunguka kuhusu wimbo wake mpya 'Popstar.' 

•Vera alifichua kuwa mumewe alihusika sana katika wimbo wake mpya ambao aliachia siku chache zilizopita.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika alikuwa mgeni wetu katika kipindi cha Bustani la Massawe, kitengo cha Ilikuaje? mnamo siku ya Ijumaa.

Katika mahojiano na Massawe Japanni, rapa huyo mpya zaidi mjini alifunguka kuhusu wimbo wake mpya 'Popstar.' 

Mama huyo wa binti mmoja wa mwaka moja alifichua kuwa yeye na mumewe Brown Mauzo wanamiliki studio nyumbani.

"Tuko na studio nyumbani ili tuweze kufanya kazi kwa siri. Mume wangu anarekodi nyimbo zake nyumbani," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 33 alibainisha kuwa studio hiyo ni ya matumizi yao pekee yao wala si ya kibiashara. Alisema kwa kawaida huwa wanatafuta watayarishaji muziki ili wawasaidie kutengeneza muziki nyumbani

Vera alifichua kuwa mumewe alihusika sana katika wimbo wake mpya ambao aliachia siku chache zilizopita.

"Aliniunganisha na maproducer bora zaidi. Pia alikuwa kwenye video (nyuma ya pazia," alisema.

Rapa huyo aliweka wazi kuwa Mauzo ni shabiki wake mkubwa sana

"Yeye ni shabiki wangu nambari moja. Pia alinisaidia katika kiki," alisema.

Aliongeza, "Nashukuru mume wangu kwa kuwa amekuwa akinisaidia katika safari ya muziki."

Vera alifichua kuwa mchakato wa kurekodi wimbo wake 'Popstar' ulichukua kipindi cha wiki moja tu.

"Nilirekodi muziki kwa siku mbili, Nilifanya kila kitu kwa wiki moja" alisema.