Mwanadada amefunguka na kueleza kwamba bwana yake alikuwa anachukua nguo zake mara kwa mara na kuvalia mpaka zile za ndani.
Mwanamke huyo kwenye mahojiano na mtangazaji wa Radio Jambo Massawe Japani alieleza kwamba alikuwa anaudhika sana na tabia za mumewe kuchukua nguo zake na kwenda kucheza nazo kucheza mpira mbele ya watu na hata wakati mwingine kutembea nazo hadharani.
"Unaona hizi baika za mademu, hizi zenye hazina lens, na alikuwa mchezaji wa mpira, hizo ndizo alikuwa anachukua anavaa sasa ndio anasimama nazo kwa goli... Ile sasa amesharudi kwa nyumba ndio nashindwa bro kumbe ulienda na hii ananiambia hii ndo nilitumia kama short ya ball," alifuchua mwanadada huyo.
Aliendelea na kueleza kwamba mwanaume huyo hakuwa anavalia tu nguo za ndani pekee lakini hata suruali zake ambazo amezinunua yeye mwenyewe mume wake alikua anachukua na kutembea nazo hadharani.
"Sasa ikakuja ni surualli ya jeans, alikuwa anavaa hipster zangu. Yaani bro akitoka ameng'ara kumbe ameng'aria nguo yangu ya demu,' alieleza zaidi.
Mwanamke huyo pia alifichua kwamba baada ya kushindwa kununua mavazi yake mwenyewe na kuanza kuvalia nguo za mkewe bado aliendelea kumutesa na kumpiga kila wakati bila kukoma.
"Bro alikuwa anachapana, unasikianga kiboko. Hakununulia panti, hawezi ata kujinunulia nguo, hawezi kujinunulia boxer lakini bado anakutandika. Ashindwe popote alipo ata sai. Skini tites zangu za black alikuwa anakata inakuwa kama shoti na anavalia," aliweka wazi mwanadada huyo.
Aliendelea mbele na kueleza kwamba mwanaume huyo alikuwa kati ya yumri wa miaka 24 na 25 kwni alikuwa anamzidi na miaka kama mitatu. "Alikuwa kati ya miaka 24 na 25 maana mimi nilikuwa karibu 22" alisema.