Mwanaume mmoja amefichua kwamba ilimulazimu kurudi kwa waliokuwa wakwe watarajiwa kudai mahari aliyokuwa amepeleka baada ya ndoa iliyokuwa imepangwa kati yake na msichana wao kuvunjika kuvunjika kabla ya kuanza.
Mwanaume huyo kwenye Mahojiano na Masawe Japani kwenye Radio Jambo alikiri kwamba mahusiano hayo yalivunjika siku mbili tu kabla ha harusi ya kufunga ndoa.
Ameeleza kwamba ilimulazimu kwenda nyumbani kwa kina msichana huyo na kupeana masharti makali.
'Mimi nikaenda kwao nikawaambia sitoki hapa kabla hamjanipea pesa yangu. Hamuezi kaa na msichana na mkae na pesa yangu. Mahari ilikuwa karibu elifu 100,000. Zilikuwa elfu 70 na wakati huo sijahesabu za kupika za wageni, chakula ambacho nuilinunulia huyo mwanamke kwa ajili ya wageni zingine na kadhalika.,' alieza Mwanaume huyo kwa machungu.
Wakati huo pia aliendelea na kueleza kwamba walikuwa wamekaa kwenye mahusiano hayo kwa miezi minane na sasa walikuwa wanakamilisha mipango ya kuowana. "Tulikuwa tumechumbiana kwa muda kitu miezi minane," alisema.
Mwanaume huyo ameendelea na kufichuwa kwamba chanzo kikubwa kilichofanya mahusiano hayo kuvunjika ni tabia mbaya ya aliyekuwa mchumba wake akidai kwamba alianza mahusiano na wanaume wengine.
Alisisitiza kwamba tabia hii mbaya ilianza kuonekana kwake baada tu ya kumusaidia musichana huyo kupata kazi kwenye hoteli moja.
"Nilimutafutria kazi ya hoteli ili asikae hivyo tu bila kazi. Baada ya siku chache tu wanaume wakaanza kumusindikiza akienda nyumbani. Wanaume, sasa mimi kumukanya akasema nataka kukuacha na sasa mimi pia nikaamua kuachana na yeye," alileza zaidi mwanaume huyo.