Aliyekuwa mume wangu alimtumia mama yangu jumbe za matusi-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke asema mumewe alimtusi mama yake baada ya kuachana
Teke Teke:Mbusi na Lion
Image: Studio

Baada ya wapenzi na wanandoa kuachana huwa wengine huwa wanafuatana na kuacha wenzao wameangamia ili kulipiza kizazi.

KUna wale pia huvuka mipaka na hata kuwaingiza wazazi katika uhusiano wao, huku baadhi yao wakiwatusi wazazi wa wake zzao.

Mwanamke mmoja alitaka mumewe apewe Nyahunyo katika kipindi cha Mbusi na Lion kwa kumtusi mama yake baada ya wao kuachana.

"Nataka aliyekuwa mume wangu apewe nyahunyo, mama yake alinitumia ujumbe na kuniambia kwamba nahitaji maombi kwa maana niliachana na mtoto wake

Nilimjibu na kumwambia kwamba ni mwanaye anahitaji maombi wala si mimi, baada ya dakika chache  mwanaye alimtumia mama yangu jumbe akiwa amemtusi matusi mabaya ambayo hayawezi semezeka

Mimi si kumtusi mama yake lakini alikuwa na ujasiri wa kumtusi mtu ambaye alikuwa mama mkwe wake," Alieleza mwanamke huyo

Mashabiki wa Radiojambo walidai apewe Nyahunyo, je kwa maoni yako mwanamume huyo alipaswa kupewa nyahunyo?

Na je ni vyema watu wakiachana wawaingize wazazi katika ugomvi wao?