Aliyekuwa mume wangu amekuwa akinitusi kwa sababu nilimuacha-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Hamna mwanamke ambaye anatamani kuachana na mumewe au kuacha familia yake, ambayo ameijenga kwa muda mrefu
  • Mwanamke huyo alifuichua kwaba wamekuwa na mumewe kwa miaka kumi lakini waliachana mwaka mmoja uliopita kutokana na tabaia ya mumewe ya kulewa
Lion,DJ Nyce na Mbusi
Image: Studio

Katika kitengo cha Nyahunyo mwanamke mmoja alitaka mumewe apigwe nyahunyo kw tabia ambazo amekuwa akimuonyesha baaada ya kumuacha.

Hamna mwanamke ambaye anatamani kuachana na mumewe au kuacha familia yake, ambayo ameijenga kwa muda mrefu.

Mwanamke huyo alifuichua kwaba wamekuwa na mumewe kwa miaka kumi lakini waliachana mwaka mmoja uliopita kutokana na tabaia ya mumewe ya kulewa.

Baada ya kumuacha mumewe ameuwa akimtumia jumbe za matusi, kwa sababu ameshindwa kufua nguo zake chafu.

"Nataka aliyekuwa mume wangu apigwe nyahunyo kwa sababu amekuwa akinitumia jumbe akinitusi pamoja na wazazi wangu 

Nilimuacha mwaka mmoja uliopita kwa sababu alikuwa analewa chakari, na kuja nyumbani nguo zikiwa chafu sana

Naona sasa ananitusi kwa sababu ameshindwa kufua nguo zake chafu, tumekuwa naye kwa miaka kumi lakini tabia yake ya ulevi ilinishinda," Alisimulia mwanamke huyo.

Kweli msanii kutoka Tanzania hakukosea aliposema ukiachwa achika, ukitemwa temeka na ukimwagwa mwagika, kwa hivyo mwanamume huyo anapaswa kufahamu aliachwa.