Dada yangu amekuwa akinitusi kwa maana nina virusi vya ukimwi-Mwanamke asema

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi dada yake amekuwa akimtusi kwa maana ana virusi vya ukimwi
Mbusi,DJ Nice na Lion
Image: Studio

Hamna mtu ambaye anajitakia kuwa na ugonjwa, au kuwa na virusi fulani maishani mwao,ukipatikana na virusi vya ukimwi wengi humtoroka mwenye virusi hivyo.

Kuna wale hupokea kejeli kutoka kwa marafiki na hata kutengwa na familia katika maisha yao.

Katika kipindi cha nyahunyo na Mbusi na Lion teketeke, mwanake mmoja alitaka dada yake  apigwe nyahunyo kwa maana amekuwa akimpa maneno makali na kumtusi kwa maana ana virusi vya ukimwi.

Pia amekuwa akimpa mtoto wake unyanyapaa kwa maana mama yake ana virusi hivyo, kulingana na mwanamke huyo wamejaribu kutatua shida hiyo ata kuenda kwa wahubiri na polisi lakini hajaweza kusikia.

"Nataka dada yangu mdogo apigwe nyahunyo kwa sababu amekuwa akinitusi kwa muda kwa maana nina virusi vya ukimwi

Licha ya hayo yote pia amekuwa akimpa mwanamgu unyanyapaa,tumejaribu kutatua kile chote tuliweza lakini hajabadilika," Alisema mwanamke huyo.

Kwa wale wanatabia kama hiyo wanapasa kukomesha kwani hamna mtu huchagua kuwa mgonjwa au kupata virusi fulani.