Nyahunyo:Mama yangu hajawahi nionyesha baba yangu mzazi

Muhtasari
  • Mama yangu hajawahi nionyesha baba yangu mzazi
  • Ni uchungu sana kuishi bila kujua baba yako mzazi kam yuko hai
Mbusi na Lion

Ni haki ya kila mtoto kumfahamu baba yake mzazi au mama yake mzazi, lakini asilimia kubwa ya watoto na watu hawafahamu baba yao mzazi kwani wazazi wao wa kike wamekataa kuwaambia wala kuwaonyesha.

Ni uchungu sana kuishi bila kujua baba yako mzazi kam yuko hai.

Mwanamume mmoja katika kitengo cha Nyahungyo na Mbusi na Lion Teketeke alitaka mama yake apewe nyahunyo kwa kutomuonyesha baba yake mzazi.

"Nina miaka 20 sasa, nilifahamu kuwa nina tabia tofauti na mama yanu na pia baba yangu, nilipoona hayo nilienda kwa nyanya yangu kumuuliza baba yangu ni nani 

Aliniambia kwamba mwanamume na mtu ambaye namuita bab yangu sio baba yangu mzazi,niliuliza mama yangu nani baba yangu lakini akadinda kuniambia," Alieleza.

Swali kuu kwa wazazi je mtoto wako anafahamu baba yake mzazi, na kama wewe ni mwanamume je unajua kuwa mtoto anayekuita baba ni mtoto wako?