Nyahunyo:Baba yangu ana mazoea ya kumwaga chakula akiwa amelewa

Muhtasari
  • Kaika kitengo cha Nyahunyo na Mbusi na Lion teketeke mwanamume mmoja alitaka baba yake apigwe nyahunyo baada ya kuwa na mazoea ya kumwaga chakula akilewa
DJ Slim,Lion na Mbusi
Image: studio

Kaika kitengo cha Nyahunyo na Mbusi na Lion teketeke mwanamume mmoja alitaka baba yake apigwe nyahunyo baada ya kuwa na mazoea ya kumwaga chakula akilewa.

Bwana Mutuma alisema kwabma Mapema wiki hii, baba yake alifika nyumbani akiwa amelewa chakari na kumwaga githeri iliyokuwa na matumbo.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nataka baba yangu apigwe nyahunyo kwa maana anamazoea ya kumwaga chakula akiwa amelewa na endapo amekosana na mama yangu

Alianza hiyo tabia nikiwa na umri wa chini, mapema wiki hii alimwaga githeri na matumbo ambayo mama yangu alikuwa ametayarisha

Tulilala njaa mimi na ndugu yangu," Alieleza Mutuma.

KUna baadhi ya watu ambao wana mazoea ya kuharibu vitu kwa nyumba baada ya kuwa na hasira na kusababisha hasara kubwa, ndio maana wahenga walisema hasira hasara.

Wanajambo waliamua mzee huyo apewe nyahunyo ili arekebishe taba yake.