Je una mtu ambaye ana tabia mbovu au amekosea jamii, haya basi husitie shaka kwani unaweza mleta katika kipindi cha nyahunyo ili atolewe makosa yake.
Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa na tabia za kusikitisha na hata kukosea jamii bila ya kujali matokeo yake.
Mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Nairobi alitaka mumewe atolewe makosa baada ya kuwa na tabia ya kula chakula cha mtoto wake.
Kulingana na mwanamke huyo, mumewe amekuwa akila chakula cha mtoto wao ambaye ana miezi tisa
"Mume wangu amekuwa akila chakula cha mtoto wetu, nikimuuliza kwanini anafanya hivyo ananiambia kwamba anataka kuonja
Pia amekuwa akiamka usiku na kulamba asali ya mtoto, anasema kwamba anataka kujua kama ni kali au la
Nataka apewe nyahunyi awache tabia hiyo, kwa maana hanunui chakula ya mtoto lakini anakula hayo yamekuwa mazoea yake," Alisimulia mwanamke.
Je mwanamume huyo alihitaji kupewa nyahunyo au la?