Nyahunyo:Mama awekelea waliofuga rastas ni wezi

Muhtasari
  • Kuna dhana potovu na mawazo mabaya ambayo watu weng wamejaza akilini mwao kwamba watu wenye rastas sio wazuri
  • Wengi wamekuwa wakiekelewa kwamba ni wavuta Bhangi na hata wezi

Kuna dhana potovu na mawazo mabaya ambayo watu weng wamejaza akilini mwao kwamba watu wenye rastas sio wazuri.

Wengi wamekuwa wakiekelewa kwamba ni wavuta Bhangi na hata wezi.

Ni dhana ambayo watu engi wanapaswa kuifuta akilini mwao kwani, sio wote ambao ni wabaya.

Katika kitengo cha nyahunyo jamaa mmoja alitaka mama, na amabye ni jirani yake apewe nyahunyo kwa dhana hiyo potovu.

"Nataka mama ambaye ni jirani yangu apewe nyahunyo kwani amekuwa akikejeli watu ambao wamefuga rastas

Mama huyo aliibiwa juzi na kushuku kwamba ni sisi ambao tumefuga rastas, mpaka alitupeleka polisi, ilhali hakuwa na ushahidi wowote kwamba ni sisi tumeiba bidhaa zake

Tulimpeleka kwa chifu, ili awache tabia hiyo lakini bado hajakoma, nataka apewe nyahunyo kwa kuwekelea watu ambao wana rastas makosa ambayo hawajafanya," Alisema

Haya yanajiri, siku chache baada ya wanaume 4 kuuawa na raia Kitengela wakidhaniwa ni wezi wa ng'ombe kwani walikuwa na rastas.

Hya ni mawazo ambayo watu wanapaswa kuyatoa akilini mwao, kwani hatupaswi kuhukumu watu jinsi walivyo.