Nyahunyo:Jamaa ana mazoea ya kumchungulia jirani yake akifanya tendo la ndoa na mpenziwe

Muhtasari
  • Jamaa ana mazoea ya kumchungulia jirani yake akifanya tendo la ndoa na mpenziwe

Wakikosea jamii au wakikukosea haya basi walete kwenye radiojambo, kitengo cha nyahunyo wapewe adabu.

Jamaa mmoja kutoka Rongai alimtaka jirani yake apewe nyahunyo kwani amekuwa na mazoea ya kumchungulia endapo ana mpenzi wake.

"Nataka Kim apewe nyahunyo kwani ana taia ya kunichungulia nikifanya tendo la ndoa na mpenzi wangu

Tunaishi kwa nyumba ya mabati, ametoboa shimo ya kunichunguliwa masaa hayo yakifika, hana bibi, lakini tabia yake inasikitisha sana," Alieleza Mwanamume huyo.

Kwa wanaoishi nyumba ya mabati, wanaweza kuthibitisha kwamba hamna siri yryote, kwani kile unafanya nyumbani kwako jirani yako huwa anaskia au wenye tabia kama ya KIm wanatoboa shimo ya kuchungulia.

Je umewahi patana na majirani wenye tabia hiyo? na jamaa huyo alistahili kupewa nyahunyo au la?