Wakikosea jamii au wakikukosea hatujakuwa tukiwaacha huru,bali tumekuwa tukiwapa nyahunyo ili warekebishe tabia zao.
Sio mmoja au wawili ambao wamekuwa wakitolewa makosa baada ya kukosea jamii au wenzao.
Siku ya Jumatano mama mmoja alimtaka katibu au karani wa shule ya msingi ya milimani kwani amekuwa akila na kuvyonza karo ya wanafunzi wa shule hiyo.
Kulingana na mwanamke huyo karani huyo amekuwa na mazoea ya kuwaambia wazazi kwamba hawajamaliza kulipa karo ya shule licha yake kupewa pesa.
"Nataka karani wa shule ya msingi ya Milimani apewe nyahunyo kwa sababu amekuwa na mazoea ya kuvyonza karo ya wanafunzi licha ya kulipwa na wazazi
Tumewasilisha malalamiko kwa mwalimu mkuu, na kutumabia kwamba atamfuta kazi, lakini tunampata hapo, ana sema kwamba hajaandikwa kazi na wazazi bali na usimamizi wa shule." Alieleza.
Je alistahi nyahunyo au la?