Mpangishaji achapwa nyahunyo kwa kuwadhulumu wapangaji

Muhtasari
  • Kulingana na jamaa huyo mpangishaji wao amekuwa akikata umeme na maji baada yao kutonunu bidhaa kwenye duka lake
(Kushoto)Mbusi,(kati)DJ Nyce,(kulia) Mbusi
Image: Studio

Wakifanya tabia mbaya tunawachapa,wakifanya ujinga,  uzembe na upuzi tunawachapa, ata makosa tunachapa nyahunyo.

Katika kitengo cha nyahunyo jamaa alimtaka mpangishaji wake apewe nyahunyo baada ya kuwadhuumu wapangaji wake.

Kulingana na jamaa huyo mpangishaji wao amekuwa akikata umeme na maji baada yao kutonunu bidhaa kwenye duka lake.

Haya hapa malalamishi yake;

"Nataka mpangishaji wa jumba ambalo naishi apewe nyahunyo kwani amekuwa na tabia isiyofurahisha, amekuwa akiwadhulumu wapangaji wake

Hii ni baada ya wapangaji wake kutonunua bidhaa katika duka lake, anazima stima na maji, tukilalamika anasema kwamba tunapaswa kuhama mwezi wa Desemba, la sivyo wapangaji wake wanunue kwenye duka lake," Alieleza Jamaa huyo.

Je umeahi ishi kwa nyumba kama hiyo, na ushauri wako kwa wapangishaji wenye wivu ni upi, na je mpangishaji huyo alistahili nyahunyo?