Nyahunyo:Dada yangu anabugia pombe ilhali yuko kidato cha pili

Muhtasari
  • Wakikosea jamii au wakikukosea hatujakuwa tukiwaacha huru,bali tumekuwa tukiwapa nyahunyo ili warekebishe tabia zao
Mbusi,DJ Nyce na Lion
Image: Studio

Wakikosea jamii au wakikukosea hatujakuwa tukiwaacha huru,bali tumekuwa tukiwapa nyahunyo ili warekebishe tabia zao.

Sio mmoja au wawili ambao wamekuwa wakitolewa makosa baada ya kukosea jamii au wenzao.

Ni matamanio ya kila mwanafamilia hasa dada yako kukuona ukiendelea vyema na masomo yako na wala sio kupoteza njia zako kama mwanafunzi.

Mwanadada mmoja alitaka dada yake ambaye yuko katika kidato cha pili apigwe nyahunyo kwa kuwa mlevi, sio hayo tu mwanafunzi huyo amekuwa akitembea na wanaumee ambao wamemzidi umri kulingana na mwana dada huyo.

"Nataka dada yangu apewe nyahunyo kwani ameshinda ata mama yangu, amekuwa akiena shule kisha anatoroka, pia amekuwa akilewa sana ana ana umri wa mika 16, pia amekuwa akitembea na 'wababa' wakubwa kushinda umri wake ambao wanalewa naye."