Nyahunyo:Jamaa achapwa nyahunyo kwa kumng'olea mpangaji wake mlango

Muhtasari
  • Wakikosea jamii tunachapa nyahunyo, wakikukosea tuna chapa, wakifanya tabia mbaya tunachapa nyahunyo
Image: Radiojambo

Wakikosea jamii tunachapa nyahunyo, wakikukosea tuna chapa, wakifanya tabia mbaya tunachapa nyahunyo.

Baada ya janga la corona kuripotiwa nchini kila mwananchi aliathirika kwa njia moja au nyingine, huku wenye nyumba wakiwasukuma wapangaji kulipa kodi ya nyumba.

Katika kitengo cha nyahunyo, mwanadada mmoja kutoka Malindi alitaka mwenye nyumba ambaye alifahamika kama Omar atolewe makosa kwa kumng'olea mpangaji wake mlango, kwa maana hakuwa amelipa kodi kwa mwezi mmoja.

"Nataka mwenye nyumba atolewe makosa kwa kumng'olea mpangaji wake mlango kwa sababu hakuwa amelipa kodi ya nyumba kwa mwezi mmoja

Licha ya hayo yote alipewa pesa ya kodi akakataa, na wapangaji hao walikuwa na mtoto mchanga."

Licha ya kuwa na haki ya kutaka haki ya kulipwa kodi wanajambo waliamua kwamba Omara ana makosa.