Nyahunyo:Jamaa atolewa makosa kwa kufanya ngono na mke wa binamu yake

Muhtasari
  • Jamaa atolewa makosa kwa kufanya ngono na mke wa binamu yake
Lion,DJNyce na Mbusi
Image: Studio

Wakifanya tabia mbaya tunawachapa,wakifanya upuzi tunawachapa,uzembe na upuzi tunachapa nyahunyo hata makosa tunachapa nyahunyo, katika kitengo cha nyahunyo.

Vitendo vya kutisha usinzi umekuwa ukienea kila kona mwa nchi hasa katika karne hii ya sasa.

Baba hajali kuwa ana msichana na kisha kumbaka na hata kumnajisi,licha ya kuwa ni mwanawe, pia akina mama hawajali kuwa mwanamume ambaye anajitimizia mahitaji yake ya ndoa ni mwanawe.

Utawapata akina mama wanawachumbia wanaume wenye umri na mtoto wake, huku wasichana wakichumbiana na akina baba ambao wana umri mmoja na baba yake mzazi.

Katika kipindi cha nyahunyo siku ya Jumatano, mwanamume mmoja alimtaka binamu yake apigwe nyahunyo kwa kufanya ngono na mkewe mtarajiwa.

"Nataka binamu yangu apewe nyahunyo kwa kufanya ngono na mke wangu ambaye nilikuwa natarajia kumuoa, hii ni tabia ambayo haistahili kamwe," Alisema Jamaa huyo.

Ndani ya #Nyahunyo Jamaa anadai cousin yake alifanya ngono na bibi yake ambaye alitarajia kumuoa. Una ujumbe upi kwake? Sms 22494

Posted by Radio Jambo on Wednesday, April 20, 2022