PATANISHO:Nilikosana na ndugu yangu baada ya mke wake kuleta vitina

Muhtasari

•Nilikosana na ndugu yangu baada ya mke wake kunitusi

•Nilikuwa namfanyia kazi eneo la Limuru

•Mke wake alileta vitina

•Nilijitenga na mambo yake na kurudi nyumbani

Gidi na ghost
Gidi na ghost Gidi na ghost
Image: radiojambo

 

Bwana Benson alituma ujumbe ili apatanishwe na ndugu yake mkubwa Joseph baada ya yake kuamini vitina vya mkewe.

Huku akieleza usimulizi wake bwana Benson alikuwa na haya ya kusema,

 

"Nilikuwa nafanyia ndugu yangu kazi baada ya muda mkewe alileta vita huku akisema ya kwamba hataki tuishi pamoja

nilifuganya virago na kuenda nyumbani baada ya kufika nyumbani mke wake alinipigia simu na kusema ya kwamba nilisema kuwa yeye ni mchawi na ni malaya na kunitusi vibaya sana

kutoka siku hiyo sijawahi ongea na ndugu yangu kwa maana alisema kuwa hataki kuzungumza nami

nataka tupatanishwe naye kwa maana ni yeye mkubwa wa boma na tunapaswa kukuangalia na kufuta nyayo zako." Alieleza Benson.

Baada ya Joseph kupigiwa simu alisema kuwa;

"Mimi sina shida na wewe na wala sina kinyongo nawe, ninampenda sana lakini wewe ulikuwa na hasira na kusema mke wangu ameniroga

Sina shida naye kabisa kwa maana ni ndugu yangu mdogo na nimemlea, nataka tuishi kama ndugu." Alisema Joseph.

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao yetu ya youtube.