PATANISHO:Mke wangu alitolewa kwa ndoa na dada yake

Muhtasari
  • Mke wangu alitolewa katika ndoa yetu na dada yake
  • Mimi simpendi Ken na sitaki kuzungumza naye
  • Mimi nimemfungulia njia kwa wale wote walikuwa wanadhani niko nayo pia mimi nimerudi kwa kiwanja
Gidi na Ghost
Image: Radiojambo

Bwana Ken alituma ujumbe studioni zetu ili apatanishwe na mke wake Croline ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka sita ilhali dada yake alimshawishi atoke katika ndoa yake mwaka jana Oktoba.

"Tumekuwa kwa ndoa kwa miaka sita, mimi na mke wanhu huwa tunakosana kwa sababu ya shida za kinyumbani lakini tunasuluhisha

Mwaka jana dada yake alimwambia atoke kwenye ndoa, nahisi kuwa dadake hanipendi, lakini nahisi mke wangu bado ananipenda

 

nataka kujua kama ile upendo alikuwa nao nilipomuoa,nataka aniambie mbele ya wakenya kama hanipendi ama ananipenda

nitashukuru uamuzi wake, kwa maana mimi nampenda sana na moyo wangu wote." Alieleza Ken.

Tulipofanya juhudi zetu za kumfikia Mkewe Caroline Chebet alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi sitaki kuzungumza naye na simpendi kabisa." Caroline Alisema.

Baada ya kuzungumza hayo Ken alisema kuwa wamebarikiwa na mtoto mmoja ambaye anaishi na mama yake ken.

Je utampa ushauri upi kuhusu mtoto wake?