logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO:Alinipata na mwanamke mwingine lodging na kuniacha-Dismus

Nilipatwa na shetani kidogo,niliachana na huyo mwanamke hiyo siku ambayo tulifumaniwa,

image
na Radio Jambo

Yanayojiri23 October 2020 - 05:42

Muhtasari


  • Mke wangu alinifumania na mwanamke lodging
  • Ni shetani alinijaribu kidogo kwa maana ni mara ya kwanza kufanya hayo

Hii leo katika kitengo cha patanisho bwana Dismus alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe Winfridah ambaye alimuacha baada ya kumfumania na mwanamke mwingine lodging miezi mitano iliyopita.

Huu hapa usimulizi wake;

"Mke wangu alinipata lodging na mwanamke mwingine, na tulikuwa katika burudani, sijawahi danganya au kuenda nje ya ndoa lakini ndio nilikuwa nataka kuanza

 

Nilipatwa na shetani kidogo,niliachana na huyo mwanamke hiyo siku ambayo tulifumaniwa, niliporudi nyumbani nilimpta mke wangu ameenda kwao."

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia mkewe simu naye kwa upande wake alikuwa na haya ya kusema.

"Nilikuwa nimesika mara nyingi kuwa mume wangu alikuwa anaenda nje ya ndoa siku moja rafiki yangu aliniambia kuwa mume wangu yuko katika lodging na mwanamke nilipoenda nilimpata na mwanamke mwingine wakiwa katika hali ya kimapenzi

Itakuwa vigumu sana kurudiana, lakini nishaa msamehe kitambo,atanitafuta tuongee zaidi kuhusu mambo hayo."

Kwa mengi zaidi tembelea youtube ya Radiojambo kwa uhondo zaidi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved