PATANISHO:Nilikosana na mama mkwe baada ya kumkubali mke mwenza wangu kwake

Muhtasari
  • Mume wangu aliniletea mke wa pili, huku akienda kukaa na mama mkwe
  • Niliambia mama mkwe ata akiletewa wakwe wenza 100 awapokee
Gidi na Ghost

Katika kitengo cha patanisho Bi Stella Kawira alituma ujumbe ili apatanishwe na mama mkwe ambaye walikosana miaka miwili iliyopita baada ya kukubali kukaa na mke mwenza.

"Mume wangu alioa mke mwingine na akaanza kunitesa huku akinichapa, nilipolalamika mume wangu alimfukuza na mke mwenza akaenda kwa mama mkwe

Nilipompigia mama mkwe simu na kumuuliza kwanini alikubali mke mwenza ilhali anajua mtoto wake ana mke na watoto aliniambia akiletewa ata kaa nawao na mimi nilimwambia akitaka apelekewe wakwe wenza 100 na aandike masaai awalinde

 
 

Kisha aliniambia kuwa hawafahamu watoto wangu, na ni kweli kwa maana baada ya kujifungua hajawahi kuja kuniona

Nataka nipatanishwe naye kwwa maana naona nilimkosea kama mtoto kwa matamshi ambayo nilimwambia." Aliongea Stella.

Baada ya kufanya juhudi za kumpigia mama mkwe naye kwa upande wake alikuwa na haya ya kusema.

"Mimi sina shida nimekusamehe, ubaya huwa hautembei huku nyumbani, karibu nyumbani nimekukaribisha wakati wowote," Alisema Mama Ken.

Stella alifurahi sana kwa kupata msamaha kutoka kwa mama mkwe huku akiahidi atamtembelea ili waweze kuzungumza.