Nilikosana na mke wangu kwa sababu sina pesa mimi ni hustler

Muhtasari
  • Bwana yangu huwa akipata pesa anahesabia kwa bafu
  • Mke wangu aliniacha kwa maana sikuwa na pesa
Gidi na Ghost

Bwana Abraham alituma ujumbe apatanishwe na mke wake ambaye walikosana naye wiki mbili zilizopita.

"Nilioa mke wanu mika miwili iliyopita, mimi sina kazi mimi huwa nafanya vibarua yaani mimi ni hustler, siku moja nilitoka kuenda kutafuta kazi niliporudi nilipata amerudi kwao na wala hakuniambia sababu lakini najua ni kwa ajili sina pesa." Alieleza Abraham.

Baada ya kyfanya juhudi zetu za kumigia mke wake simu alikuwa na haya ya kusema,

 

"Huyu mwanamume likuwa ananiacha nyumbani bila chakula wala pesa, akipata pesa anahesabia kwa bafu alafu ananiletea badala anipe pesa kama mwanamk wa nyumba ni nunue bidhaa yeye mwenyewe anaenda kununua 

Anitumie nauli basi nirudi."

Mkewe Abraham alikata kauli hiyo baada ya Abraham kuomba msamaha, je maoni yako ni yapi?