Patanisho:Wazazi wangu wanasema si vyema kwenda kwa mke wangu

Muhtasari
  • Ochieng alimuoa msichana wetu akiwa na miaka,16 kinyume cha sheria
  • Wazazi wangu wanasema si vyema kuenda kwa mke wangu
patanisho
patanisho

Bwana Ochieng,32, alituma ujumbe apatanishwe na mama mkwe baada ya yake kuchukua mke wake na kumwambia aende kuishi nao.

"Nilifungiwa nyumba mara ya kwanza mara pili niliona wacha nitoke mapema ili vitu vyangu visifungiwe, bibi yangu Sonya alienda kwao na wazazi wangu wanakataa niende huko kwa maana si vyema katika mila zetu." Alieleza Ochieng.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia mama mkwe alisema kwamba Ochieng huwa anamtesa msichana wao kwa maana Sonya amekuwa akifanya vibarua vya kufua na kupata pesa za chakula.

Baada ya kupata pesa za vibarua mama huyo alidai kuwa amekuwa akimnyang'anya mkewe pesa hizo huku akiwa mlevi.

"Msichana wangu ana shida nyingi sana huyu kijana ni muongo kwa maana tulimpigia simu jana aje tuzungumze na kutatua shida yao lakini anatupeleka radiojambo

Amekuwa akinywa vileo na kumpiga mke wake, kwanza alimpa Sonya mimba akiwa na miaka,16,sasa ndio anafikisha miaka 18, tungetaka tungempeleka ndani kwa maana amevunja sheria

Mimi nataka waje wasikizane na tutatue shida hatutaki aje kukaa huku, tunampenda na licha ya shida ambazo wanapitia kuna siku Mungu atawakumbuka na kuwabariki." Alizungumza mama Mkwe.

Mama mkwe alitupilia mbali madai ya kwamba Sonya amekuwa kwao kwa wiki moja huku akisema ameishi hapo kwa siku tatu.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.