Patanisho: Ni kama mke wangu aliniwekelea mtoto kwa maana hanifanani

Muhtasari
  • Nilikosana na mke wangu baada ya yake kuenda kwa dada yake
  • Nikama aliniekelea mimba kwa maana mtoto hanifanani anafanana mama yake
  • Odhiambo hajui sura ya mtoto, mtoto ni wake
  • Nimemuachilia huru kwa maana tayari ashaa oa
Gidi na Ghost
Gidi na Ghost

Bwana Odiambo alituma ujumbe ii apatanishwe na mkewe Susan ambaye walikosana naye miaka mitatu iliyopita.

"Nilikosana na mke wangu baada ya yeye kuenda kwa dada yake baada ya muda ndugu yake aliaga dunia na  nikawatuma wazazi wangu kuhudduria mazishi, mazishi yalipokamilika nilimpigia simu na kuniambia kuwa atakuja

Kwa miaka hiyo yote amekuwa nikimtumia nauli anafunga simu, na kuniambia kuwa anatakuja tu

Hata ni kama ameniekelea kuwa mtoto aliye naye ni wangu kwa maana anamfanana." Aliongea Odhiambo

Baada ya kumpigia mkewe alikuwa na haya ya kusema.

"Hjawahi nipigia simu alinitumia ujumbe jana na kuniambia ni rudi, kwanza mambo ya kwao yamenichosha kabisa na sitawahi rudi

Kwanza anazungumza ilhali ameoa mimi nimemueka huru aendelee na maisha yake mimi sirudi kwake kwa maana mwaka ujao nataka kurudi shule

Anadai amewahi ona mtoto ilhali nilitoka kwake nikiwa na mimba hajawahi ona mtoto." Alisema Susan.