Patanisho: Mume wangu amekuwa akizungumza na ex wake ilhali ameolewa

Muhtasari
  • Mume wangu amekuwa akizungumza na ex wake ilhali ameolewa
  • Bi Lilian na Joseph wamekuwa kwa ndoa kwa muda wa miaka miwili
zawadi
zawadi

Leo katika kitengo cha patanisho Bi.Lilian alituma ujumbe apatanishwe na mumewe Joseph ambaye hawaongeleshani kwa maana mumewe amekuwa akizungumza na alyekuwa mke wake.

"Mume wangu amekuwa akizungumza na ex wake, kuna siku ambayo walikuwa wanazungumza kwenye facebook, baada ya hapo wanaoigiana simu kwenye whatsapp

nilipomuuliza anasema ya kwamba alikuwa anamuuliza bei ya dengu, ni jambo ambalo linaniumiza sana moyo, pia nilimpata amepakia picha za eex wake kwenye mitandao ya whatsapp licha ya kuwa ex wake ameolewa." Alieleza LIlian

 

Wawili hao wamekuwa katika ndoa kwa miaka miwili, baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia bwana yake alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi niliambia mke wangu kuwa ni yeye tu na hakuna mwingine mimi sina haja na e wangu kwa maana ameolewa na pia aliyekuwa mke wangu alimwambia kuwa hana haja nami

Nampenda tu mke wangu na hakuna mwanamke mwingine." Joseph Alisema.

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.