PATANISHO:Mke wangu aliniacha baada ya kugundua ndugu yangu mdogo amekuwa akimtumia pesa

Muhtasari
  • Ni kama nilikuwa  kijakazi wake na mlinzi wake kwa maana sijapata chochote katika ndoa hii wacha tu mtoto
  • Mke wangu alienda baada ya yangu kumuuliza kwanini amekuwa akitumiwa pesa na ndugu yangu mdogo
Gidi na Ghost

Leo katika kitengo cha patanisho bwana Masinde alituma ujumbe apatanishwe na mkewe ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka mitano na walikosana wiki jana baada ya kugundua mkewe amekuwa akitumiwa na ndugu yake mdogo.

"Wiki jana nilikuwa na simu ya mke wangu , kuangalia simu yake amekuwa wakizungumza na ndugu yangu mdogo na kuwa amekuwa akimtumia pesa nilipomuuliza alikasirika na kuenda kwao

Tumebarikiwa na mtoto mmoja." Alieleza Masinde.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia mkewe Nancy simu alikuwa na haya ya kusema;

"Sitaki mambo ya huyu mwanamume, kwani bibi ambao alikuwa anawaleta nyumbani amewakataa, ndugu yake alikuwa ananitumia pesa ya matanga na wala hajawahi nitumia pesa

Kila mwaka maisha ni yale yale, kukosana kila wakati ni kisirani aliniambia kwamba mimi ni bibi wa familia

Mimi ni malaya aoe watu watakatifu kwa maana mimi si mtakatifu, ni kama nilikuwa mlinzi wake kwa maana amekuwa akikuja nyumbani saa sita ya usiku

Mimi nikama nilikuwa kijakazi wake, mimi simtaki nimempea ruhusa aweze kuoa na mimi nitatafuta mwanamume wa kuoa kama ni mtoto ambaye unataka kuja umchukue."

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.