PATANISHO: Mume wangu aliniletea nguo akiwa amepaguzia uchafu wa mwanamke

Muhtasari
  • mume wangu amekuwa akinitesa sana naomba mnipatanishe ili abadilike
  • Juzi aliniletea shati likiwa na uchafu wa mwanamke
  • Shati hilo haikuwa na uchafu wa mwanamke ilikuwa dawa ya meno
Gidi na Ghost

Leo katika kitengo cha patanisho Bi Linet alituma ujumbe ili apatanishwe na mumewe ambaye wamekuwa wakikosana kwa muda.

"Tumekuwa kwa ndoa kwa miaka kumi na nne, mume wengu ni makanga amekuwa akirudi nyumbani akiwa amelewa chakari, hivi juzi aliniletea shati lake likiwa na uchafu wa mwanamke ili nioshe

Nikimuuliza anapinga kila kitu nikimpelekea kwa wazazi ili wazungumze naye ili abadilike baba yake anakuwa uoande wake wanaanza kubugia vileo pamoja." Alieleza Linet.

Kwa upande wake bwana Timothy alikuwa na haya ya kueleza;

"Mimi nilimuoa huyu mwanamke nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii ili kupata riziki ya kila siku, amekuwa akisikiza manaeno ya watu wengine, hakuna siku ambayo nimelala nje shati ambalo anasema nilipiga mswaki nayo na nikajipangusia dawa huo haukuwa uchafu wa mwanamke

Hii kazi yetu huwa tunafunga usiku nikimaliza naenda nyumbani nafika napata mama amekasirika vibaya." Alisema Timothy.