PATANISHO:Nilikosana na mke wangu baada ya mimi kwenda nje ya ndoa

Muhtasari
  • Nilipata mpango wa kando kaunti zilipofungwa kwa ajili ya kuthibiti kusambaa kwa virusi vya corona
  • Mkewe Julius alisema kwamba imekuwa ni mazoea kwa mumewe kukuwa na mipango wa kando

Bwana Julius,30, alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe ambaye wamekuwa katika ndoa kwa miaka kumi.

"Wakati nchi na kaunti zilikuwa zimefungwa kwa ajili ya kuthibiti kusambaa kwa corona, nilipata mpango wa kando baada ya kufunguliwa mke wangu alifahamu kuwa nilikuwa na mpango wa kando

Aliambiwa na marafiki zangu ambao waliniona naye, tumebarikiwa na watoto watatu." Alisema JUlius.

 
 

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia mkewe Elizabeth alisema kwamba imekuwa mazoea ya mumewe kufanya hayo na kuenda nje ya ndoa;

"Mimi nilimsamehe  kitambo, lakini imekuwa mazoea kwa maana amekuwa akifanya hayo nikijua mpango wake wa kando anamuacha na kuenda anatafuta mwingine huku akiniambia ya kwamba atabadilika lakini habadiliki

Mume wangu aliniambia nikae mashambani aende kazi kumbe yeye anaenda kutafuta wanawake wengine." Alisema Elizabeth.