PATANISHO:Mke wangu amekuwa akienda kulala nje nikienda kazini

Muhtasari
  • William alisema kwamba mkewe huwa anaenda nje akienda kazi usiku
  • Mkewe naye alisema kwamba mumewe hajakuwa akijukumikia mahitaji ya nyumbani huku ikimlazimu kutafuta kazi
Gidi na Ghost

Bwana William Rono alituma ujumbe apatanishwe na mkewe ambaye alidai alikuwa anaenda nje ya ndoa.

"Nimekuwa nikienda kazi usiku, nikirudi nyumbani nampata mke wangu hayuko, nimefanya uchunguzi na kujua kuwa nikitoka usiku nikienda kazini anatoka anaenda." Rono Alieleza.

Baada ya mkewe Faith kuzungumza kuhusu madai hayo alikuwa na haya ya kusema,

 

"Rono hajakuwa akijukumika nyumbani, hata hajui watoto wanakula nini au penseli ni pesa ngapi

Ni mimi nimekuwa nikitoka nje na kutafuta kazi ili watoto wangu wawezze kula na kutimiza mahitaji yao

Nikipigiwa simu lazima aangalie ni nani anachukua namba ya simu anamtumia mama yangu,endapo nimemuitisha pesa ya kununua bidhaa za nyumbani huwa ananitetesha

Tangu watoto waende nyumbani hajwahi tuma hata shillingi moja hajui watoto wanakula nini, ndio alinioa nikiwa na mtoto mmoja na tukabarikiwa na wengine wawili

Nimechoka sasa staki mambo yake." Faith Aliongea.