Katika kitengo cha patanisho hii leo Bi Maureen alituma ujumbe apatanishwe na mume wake ambaye walikosana naye baada ya yake kusema kuwa anatoka nje ya ndoa.
"Nilikosana na mume wangu baada ya kuenda kuhudhuria mazishi kwao, alinipigia simu na kuniambia kuwa nisirudi nyumbani
Nilimpa mama yake simu wakazungumza, niliporudi nyumbani alinichapa mpaka pua langu likaanza kutokwa damu
Niliwarudisha watoto wangu kwao." Alieleza Achieng.
Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mumewe James alikuwa na haya ya kusema;
"Mimi sitaki mambo ya huyu mwanamke amekuwa akihanya kila mara na wanaume wengi, kwa maana mimi ni maskini amekuwa akienda kuhanya nje na kurudishwa nyumbani na magari
Anasema anaishi kwa dada yake, huyo dada yake alinipigia simu na kuniambia kwamba nisirudiane naye wa maana amepata mwanamume wa kuoa
Wacha hao wanaume wako na magari wakuoe, ujipodoe uvalia nguo fupi fupi uwaonyeshe kila kitu, mimi sitaki kuoa niko sawa hivyo
Ataomba msamaha arudi na kisha baada ya miezi miwili aanze tabia yake." Alisema James.
Kwa kweli bwana huyo alikuwa na hasia na mkewe kwa maana alikata kauli kwamba hamtaki wala kumuhitaji mkewe na kwamba amemruhusu aolewe tena.
Bi Achieng alisema kwamba mumewe amekuwa akisikiza maneno ya watu hasa ya mjomba wake.