Patanisho:Niligundua kuwa mtoto wangu si wangu bali ni wa mtoto wa ndugu yangu

Muhtasari
  • Nilikosana na baba yanu baada ya yake kunisomesha lakini nikaacha shule
Gidi na Ghost

Katika kitengo cha patanisho bwana Eric Juma alituma ujumbe apatanishwe na baba yake waliokosana mwaka wa 2017 baada ya kumsomesha na kisha akakataa shule.

"Nilikosana na baba yangu aliponisomesha na kisha nikakataa shule, alinipeleka shule ya kupewa heshima lakini nilitoroka alinirudisha tena na nikatoroka tena

Baada ya kufikisha umri wa kuoa nilianza kuiba miraa ya baba yangu,ni mambo ambayo yalifanya baba yangu afukuze mama yangu." Aliongea Eric.

Baada ya kufanya juhudi za kumpigia baba yake ERic Bwana Stanley alikuw na haya ya kusema,

"Mimi si baba yako mama yako aliniambia kuwa wewe si mtoto wangu kwa hivyo siwezi kukusamehe

Baba yake Eric ni mtoto wa ndugu yangu, tulienda mpaka kwa sheria za watoto mama akaambiwa amlete mwanae lakini akakataa

Mimi siwezi msamehe kwa yale walinitendea." Aliongea Stanley.

Je unaweza wapa ushauri upi?