Patanisho:Mume wangu amekuwa akiniita malaya ilhali mimi ni mwaminifu kwake

Muhtasari
  • Mume wangu amekuwa akiniita malaya ilhali mimi ni mwaminifu kwake
Gidi na Ghost

Bwana Walter alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe Zipporah ambaye alisema walikosana Desemba mwaka jana 2020 kwa kuwa na mipango ya kando.

"Mwaka jana mke wanu alpigiwa simu na akasema ni 'wrong number' nilipofuatili nilipata kwamba mwanamume huyo alikuwa amempigia simu wanafanyakazi pamoja na wamekuwa katika uhusiano

Amekuwa na mipango ya kando, nilipomuuliza alitoka akaenda, tumekuwa kwa ndoa kwa miaka 26," Alieleza Walter.

 

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumfikia mkewe alikuwa na haya ya kusema.

"Bwana Walter amekuwa akiniita malaya tangu kitambo sana lakini mimi ni mwaminifu kwake,amekuwa akinifuata nikitoka kazini nimefika wapi, nimepanda gari ama mahali nimefika

Amekuwa na wanawake wengi mpaka huwa napokea jumbe kutoka kwao,nilieleza mama yangu shida hiyo na kuapa sijawahi fanya kitu mbaya

Amekuwa akinichunga tangu kifungua mimba wangu, akiwa na miaka miwili, sijawahi fanya umalaya amekuwa akiniekelea," Alisema Zipporah.

Pia bwana Walter alikiri kuwa amekuwa na mpango wa kando.

Zipporah aieleza na kusema kwamba Walter amekuwa akitumia tajiri wake jumbe huku akisababisha kufutwa kwake kazini.

"Amekuwa akinitishia maisha akiniambia kwamba ataniua, amefanya nifutwe kazi kwa kutumia waajiri wangu jumbe,"

Kwa mengi zaii tembela Radiojambo Youtube.