logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO:Mke wangu aliniacha baada ya kumpigia mwanamke mwigine simu

Simiyu alisema kwamba mkewe ana ujauzito wake na wamekuwa kwa ndoa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

image
na Radio Jambo

Habari17 March 2021 - 05:46

Muhtasari


  • Mke wangu aliniacha baada yangu kuongea na mwanamke mwingine
  • Simiyu alisema kwamba mkewe ana ujauzito wake na wamekuwa kwa ndoa kwa zaidi ya mwaka mmoja

Bwana Alex Simiyu alituma ujumbe  apatanishwe na mke wake ambaye walikosana wiki jana baada ya kuongea na mwanamke mwingine.

Simiyu alisema kwamba mkewe ana ujauzito wake na wamekuwa kwa ndoa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

"Nilikosana na mke wangu baada yangu kuongea na mwanamke ambaye tunafanya kazi naye, nilipoitisha namba yake mke wangu alijifanya amelala

 

nilipompigia mwanamke huyo alinyanyuka na kukasirika kisha akaenda,amekuwa akinishuku kuwa nina wanawake wengine nje," Alieleza Simiyu.

Baada ya kutafuta mkewe Rose alikuwa na haya ya kusema.

"Mwanamume huyo amenipitishia mambo mengi sana, mimi nilimsamehe licha yake kunioa hajawahi nipeleka kwa wazazi wake sijui ni mume wangu au ni nini

Sasa hivi nina ujauzito wa miezi nane, hajanunua kitu chochote cha mtoto ata suruali ya shillingi kumi

Hajui ukitaka ng'ombe itoke maziwa lazima ilishwe mzuri, kwa hivyo anapaswa kutoboka pesa, nataka afanye yote ambayo tulikubaliana  na abadilike nitarudi,"

Kwa uhondo zaidi tembelea Radiojambo youtube.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved