- Niliachana na mke wangu baada yangu kuenda kutafuta kazi na kumuacha
Bwana Geoffrey alituma ujumbe il apatanishwe na mke wake Serah ambaye amekuwa kwa ndoa naye kwa miaka 11.
Geoffrey alisema kwamba alienda kazi ghafla bila kumwambia mkewe, na tangu siku hiyo hapokei simu zake.
"Naomba mnipatanishe na mke wangu wa miaka 10. Nilienda kazi ghafla bila kumuelezea na tangu siku hiyo hapokei simu zangu
Sijawahi kurudi nyumbani tangu nipate hiyo kazi. Hata nilipata ajali nikalazwa kwa wiki 2, hakujibu hata jumbe zangu
Niliuza ng'ombe ili niende kazi," Alieleza Geoffrey.
Baada ya kufanya juhudi za kumpigia mkewe simu, Serah aliapa kutorudiana na mumewe, huku akisema amempata kwenye vyumba vya kulala na wanawake mara nyingi.
"Sitawahi kumsamehea milele na milele kwa yale amenitendea kwa miaka 11 ya ndoa. Mipango ya kando anayo mingi, anatusi hadi wazazi wangu
Kabla atoroke aliuza ndume na hakuacha hata shilingi 50. Nimemfumania mpaka 'lodging' na wanawake
tulifungiwa nyumba na nakahama sasa ndio anakuja kusema kwamba anataka kunitumia pesa, huyu mwanamume amenitendea mambo mengi na nimemuachia Mungu amtendee
nilimpata kama hana chochote tukisonga na mbele ananirudisha nyuma," Serah alisema
Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube.