Patanisho:Mume wangu alinichapa karibu meno yatoke nilipoenda kanisa

Mume wangu alinichapa baada ya kwenda kanisani karibu meno yatoke

Muhtasari
  • Katika kitengo cha patanisho bwana Victor alituma ujumbe apatanishwe na mkewe Carol ambaye walikosna na kumuachia watoto
Gidi na Ghost
Image: studio

Katika kitengo cha patanisho bwana Victor alituma ujumbe apatanishwe na mkewe Carol ambaye walikosna na kumuachia watoto.

"Nilikosana na mke wangu, na akaenda kwko nilipopigia wakwe wangu waliniambia kwamba hawajui mahali alipo bali walimtafutia kazi nairobi

Aliniacha na watoto, nikimpigia simu anasema kila wakati atarudi lakini harudi,pia niliona jumbe akiwa amemwambia mwanamume kwamba wanaweza patana nairobi kwa maana amepaa kazi huko

 

Mimi sijui ni kosa gani ambalo nilifanya ili aondokee kwangu," Alieleza Victor.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia mkewe simu alikuwa na haya ya kusema.

"Mwanamume huyo alinichapa baada ya kwenda kanisani karibu meno yatoke kutokana na kichapo ambacho alinipa

Alikuwa anasema kuwa ni yeye atanipa ruhusa ya kuenda kanisani,na pia kwamba nikienda kanisani narudi na vitina

Kurudi nitarudi Aprili 9,"