PATANISHO:Nilikosana na mpenzi wangu baada ya kumpigia msichana wake simu

Muhtasari
  • Nilikosana na mpenzi wangu baada ya kumpigia msichana wake simu

Kila asubuhi waliokosana huwa wanapatanishwa katika kitengo cha patanisho,leo katika kitengo hicho bwana nyakundi 34 alituma ujumbe apayanishwe na mpenzi wake,36.

Kulingana na nyakundi wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka 2, na wamepanga kuoana.

"Nimekuwa na mpenzi wangu kwa miaka 2, ana mimba yangu ya miezi 6,tulikosana naye baada ya kupigia mwanawe wa kwanza ambaye ni msichana simu 

Hii ni baada ya tukiwa tumekosana, na nilitaka kujua mama yake anafikiria nini kunihusu, hapo mpenzi wanu alikasirika na kuniuliza kwanini nilimpigia msichana wake simu

Na nikiona moyoni mwake amekasirika sio jinsi tulikuwa kabla ya kukosana," Alieleza bwana Nyakundi.

Baada ya kufanya juhudi za kumpigia mkewe Aggy, alikuwa na haya ya kusema;

"Mimi siwezi kukusamehe kwa maana umekuwa na madharau kila wakati,hujakuwa ukiniheshimu

KIla wakati umekuwa ukiwapigia wanawake simu na kuhanya, lakini mimi unataka kujua nazungumza na nani, lakini ukizunguma na wanawake hao unafuta jumbe zenu

Mimi sina maneno naye lakini arekebishe tabia zake, nimezoea kunikosea kisha nakusamehe," Aggy alisema.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.