Patanisho:Niliachana na mke wangu baada ya kuvuta uume wangu

Muhtasari
  • Bi Juliet aliuma ujumbe ili apatanishwe na mumewe, Macdonald ambaye waliachana miaka minne iliyopita
  • Juliet alisema kwamba walikuwa wameona kwa mwaka mmoja na nusu, na kubarikiwa na mtoto mmoja
Gidi na Ghost

Bi Juliet aliuma ujumbe ili apatanishwe na mumewe, Macdonald ambaye waliachana miaka minne iliyopita.

Juliet alisema kwamba walikuwa wameona kwa mwaka mmoja na nusu, na kubarikiwa na mtoto mmoja.

Pia alikiri kuwa mume wake alikuwa anapenda wasichana sana na ni kichwa ngumu.

"Niliachana na mume wangu kwa sababu alikuwa anapenda wasichana saana, mpaka alikuwa anataka kuwa na uhusiano na msichana wa kazi

Amekuwa akioa wasichana kisha wanaenda kwa maana hapendi kukaa na mwanamke mmoja,ntaka pia alee mtoto wetu

KUna wakati tulienda kwao nikapata ameoa mke mwingine, alikuwa ana lala nje, makosa yangu nilikuwa nampigia kelele sana," Juliet alisema.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia bwana Macdonald naye alikuwa na haya ya kusema.

"Huyu mwanamke amenifanyia mambo mengi sana, kuna wakati alikuwa anataka kuniua, pia alivuta uume wangu ndio tukaachana, amekuwa akiwatusi wazazi wangu

Amechukua pia hati zangu na kuficha,alikuwa pia anaenda kanisani kuwatusi wanawake wote ambao nilikuwa naongea na wao, alikuwa ananifuta mpaka jijini Nairobi ananivuta, nilitoka Nairobi nikaenda kukaa nyumbani kwa ajili ya hayo,"

Je nani wa kulaumiwa, kwa ajili ya kusambaratika kwa ndoa ya wawili hao? kwa uhondo zaidi tembelea Radiojambo Youtube.