Patanisho:Mke wangu aliniacha kwa sababu ya hela

Muhtasari
  • Mke wangu aliniacha kwa sababu ya hela
Ghost na Gidi
Image: Studio

Katika kitengo cha patanisho, bwana Eric alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake ambaye walikosana kwa ajili ya hela.

Kulingana na Eric wamekuwa pamoja  kwa miaka 2.

"Nilikosana na mke wangu kwa sababu ya hela. Ninafanya kazi Nairobi. Alikuwa ananunua bidhaa anaandaa chakula kisha ninakosa nafasi ya kwenda nyumbani. Akaona ninamdanganya, akapigia hesabu ya hela zote alitumia, akaniweka blacklist..."Alieleza Eric.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mkewe, alidinda kuongea na mumewe na kumpa ndugu yake simu na kumwambia kwamba Irene ameshaa endelea na maisha yake.

Morris: "Mimi ni mume wa Irene. Ambia huyo jamaa kwamba Irene ameshasonga mbele hata nina watoto naye..."

Kwa uhondo zaidi tembelea Radiojambo Youtube.