Patanisho:Mke wangu aliniacha baada ya kunipata na jumbe za wanawake

Muhtasari
  • Niliachana na mke wangu baada ya kunipata na jumbe za wanawake
Ghost na Gidi
Image: Studio

Katika kitengo cha patanisho bwana Daniel aliomba apatanishwe na mke wake, ambaye wamekuwa na yeye kwa miaka 4.

Kulingana na Daniel walikosana baada ya mke wake Catherine kumpata na jumbe za wanawake wa mitandaoni.

"Naomba nipatanishwe na mke wangu ambaye tumekuwa naye  kwa miaka 4, tulikosana baada ya kunipata na jumbe za wanawake wengine mitandaoni

Ni mwanamke mzuri na nampenda ndio maana naomba kupatanishwa naye, nilikuwa naongea na wanwake wengine kwa maana alikuwa amenipa shiinikizo sana

Nakiri nitabadilika, na kuacha kuongea na wanawake," Daniel alisema.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mkewe alikuwa na haya ya kusema kwa upande wake;

"Mimi sitaki kumuanika hewani, kwani alinikosea sana, nitamtafuta tuzungumze, kwa sasa nimekasirrika sana," Aliongea Catherine.

Je maoni yako ni yapi kuhusu patanisho ya leo?