Patanisho:Mume wangu alichapwa na mpenzi wa mwanamke wamekuwa wakizungumza sana

Muhtasari
  • Mume wangu alichapwa na mpenzi wa mwanamke wamekuwa wakizungumza sana
Ghost na Gidi
Image: Studio

Katika kutengo cha patanisho bwana Geoffrey alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe Rebecca.

Kulingana na Geoffrey mkewe alikasirika kwa kuona namba ya mwanamke mwingine kwa simu yake.

"Naomba mnipatanishe na mke wangu wa miaka 3. Aliona nambari ya simu ya msichana fulani wa nyumbani na yuataka kujua ni nani eti ninaongea naye sana. Juzi nilimwambia kwamba ni mke wangu baada ya kunishinikiza nimwambie ni nani," Alisimulia bwana Geoffrey.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mkewe alikuwa na haya ya kusema,

"Nilitaka kujua ni nani anazungumza naye kila wakti, kwa maana amekuwa akizungumza na msichana huyo kila wakati

Nilipomuuliza alikasirika, na ni mtu wa kukasirika sana, kuna wakati alitoka nje na akarudi akiwa amechapwa, kuangalia simu alikuwa amemwandikia mwanamke mwinine kwamba amechapwa na mpenzi wa mwanamke ambaye wamekuwa wakizungumza naye kwa sababu alikuwa ameenda kumtafuta."