Katika kitengo cha patanisho bwana Joseph aliomba apatanishwe na mkewe ambaye walikosana mwezi jana.
KUlingana na Joseph amekuwa akifika nyumbani amechelewa, na kumfanya mkewe akasirike huku akimtishia kuenda saudi Arabia kufanya kazi.
"Naomba mnipatanishe na mke wangu. Kulingana na kazi yangu, ninarudi nikiwa nimechelewa akaona ni kama siko serious akaondoka na sasa ananiambia hawezi kurudi na anataka kwenda kufanya kazi Saudia
Mimi nimebadilika kabisa, nitakuwa nikirudi nyumbani saa mbili, sina mpango wa kando."
Huku mkewe Phoebian akizungumzia hali hiyo na sababu yao ya kukosana alikuwa na haya ya kusema;
""Nitajuaje umebadilika?... Shida yake anakuja nyumbani kama amechelewa na nikimuuliza anakuwa mkali. Sijawahi kumshuku kuwa na mpango wa kando. Ni vigumu kurejea sasa hivi, anipe muda nifikirie. Haniheshimu kama mkewe."