Patanisho:Nilimuacha kwa sababu ya 'ujinga' wake-Kipusa atoa sababu kuu ya kumuacha mumewe

Muhtasari
  • Katika kitengo cha patanisho bwana Donald alituma ujumbe apatanishwe na mkewe bi Jackline
Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha patanisho bwana Donald alituma ujumbe apatanishwe na mkewe bi Jackline.

"Naomba nipatanishwe na mke wangu aliniacha baada yake kupata kazi, pia aliniachia mtoto wa miaka 4, sijawahi muonyesha madharau yeyote

Nataka kufahamu msimamo wake kwani aliniambia kwamba ashaa endelea na maisha yake," Alieleza Donald.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumfikia Jackline, alisema kwamba alimuacha kwani hajawahi mpeleka kwao.

"Nilimuacha kwa sababu ya ujinga wake, alinioa nikiwa na miaka 19 sasa nina miaka 23 na hajawahi nipeleka kwao

Ni mwanamume ambaye hataki nifanye kazi, nikipata kazi anabaki nyumbani akiwa amelala, sikuacha mtoto ilhali alinichapa na kuniambia niache mtoto wangu

Amekuwa akinishuku kwamba nina mpango wa kando, ilhali mwanamume ambaye anadai ni mpango wa kando wangu ni rafiki yangu kutoka nyumbani," Alisimulia Jackline.

Kwa uhondo zaidi tembelea Radiojambo Youtube.