Patanisho:Mchana peupe nilimfumania na mwanamume mwingine kitandani

Muhtasari
  • Katika kitengo cha patanisho bwana Peter 35 alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe Lydia ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 2
Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha patanisho bwana Peter 35 alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe Lydia ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 2.

Kulingana na Peter wamebarikiwa na moto mmoja, na alimfumania na mwanamume mwingine.

Huu hapa usimulizi wake;

"Naomba nipatanaishwe na mke wangu ambaye tulikosana naye mwaka huu mwezi wa Septemba, nilifumania na mwanamume mwingine ambaye ni rafiki yangu wa karibu kitandani

Nataka turudiane naye kwani tumetoka mbali naye, na licha ya yote nampenda na wala sijawahi kuwa na mpango wa kando, baada ya hayo tuligombana na akarudi kwao

Naomba afunge masikio awache kusikia mambo ya nje, nataka tuendelee na maisha," Alieleza Peter.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumfikia mkewe,hazikufua dafu kwani simu yake ilikua imezimwa.

Je ushauri wako kwa mwanamume huyu ni upi? Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.