'Sijawahi kukupenda,'Mwanadada amwambia mumewe sababu kuu ya kugura ndoa yao

Muhtasari
  • Kulingana na Alfred mke wake alikuwa anatumia muda wake mwingi kwa simu, hata kuna wakati alikuwa anajipikia
Ghost Mulee na Gidi
Image: Radiojambo

Katika kitengo cha patanisho bwana Alfred Tamba,34, alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake Akinyi ambaye walikosana tarehe 19 mwezi wa Desemba mwaka jana.

Kulingana na Alfred mke wake alikuwa anatumia muda wake mwingi kwa simu, hata kuna wakati alikuwa anajipikia.

"Mke wangu tulikosana Desemba mwaka jana baada ya kumkelelesha kwa kutumia muda wake mwingi kwa simu

Nikitoka kazi nilikuwa nikimuuliza chakula kiko wapi ananiambia naweza jipikia pia nilikuwa nikumuita tukalale anabaki akitumia simu," Alieleza Bwana Tamba.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumfikia mkewe naye alikuwa na haya ya kusema, na kueleza sababu kuu ya kugura ndoa yao.

"Nilitoka kwenye ndoa kwa sababu sijawahi kukupenda, na pia amekuwa muongo kuna mambo mengi ambayo alikuwa amenificha, kama umri wake alinidanganya kwamba ana miaka 27 kumbe alikuwa na miaka 34 

Pia alikuwa ameoa lakini hakuniambia, sababu kuu ya kutoambia wazazi wangu ni kwa maana niliona hakuna mbele wala nyuma katika ndoa hii

Nilivumilia katika ndoa kwa sababu niliona atabadilika lakini hakuweza, i don't care," Akinyi Alieleza.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.