'Nishaamove on,'Mwanamke aeleza sababu kuu ya kukosa kumrudia mumewe

Muhtasari
  • Mwanamke aeleza sababu kuu ya kukosa kumrudia mumewe
Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha patanisho bwana Keffa alituma ujumbe ili aweze kupatanishwa na mkewe ambaye walikosana naye mwaka wa 2018.

Kulingana na Keffa walikosana na mkewe baada yake kumshuku kwamba ana mpango wa kando.

"Naomba nipatanishwe na mke wangu ambaye tulikosana naye mwaka wa 2018, nimekuwa nikizungumza naye lakini amekataa turudiane

Huwa nawalipia watoto wangu karo ya shule na hata kunitemelea, sababu kuu ya kukosana alikuwa ananishuku kwamba nina mpango wa kando," Alieleza.

Je lakini haya yote ambayo ameeleza ni ya kweli huu hapa upande wa mkewe.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumfikia mkewe Njoki, alikana kurudiana naye na ameshaaendelea na maisha yake

Pia aliweka wazi kwamba alikuwa anamnyanyasa mara nyingi, na hata kumpiga, huku akikana kwamba hajakuwa akiona watoto wake.

"Siwezi rudiana naye na nimemwambia mara nyingi kwamba nishaa move on,watoto hajakuwa akiwashughulikia, alikuwa ananichapa kila mwezi mpaka meno yameng'oka, kuna wakati alikuwa anichome na gesi

Mara ya mwisho alinichapa, na kuenda na mwanamke mwingine, na ameoa wanawake wengi, lakini arudi kwa hao wanawake lakini siwezi rudiana naye."

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.