'Aliniacha kwa sababu nilikuwa nahanya,'Mwanamume akiri na kufichua sababu ya mkewe kumuacha

Muhtasari
  • Mwanamume akiri na kufichua sababu ya mkewe kumuacha
Image: RADIO JAMBO

Bwana Alphonse,27,alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake ambaye wamekuwa pamoja kwa miaka 2.

KUlingana na bwana huyo, mke wake alimuacha kwa sababu alikuwa anahanya, na kuwa na wanawake wengi.

"Naomba nipatanishwe na mke wangu ambaye tulikosana naye mwaka jana baada yangu kuhanya na wanawake wengi, nimekuwa nikimbembeleza arudi nyumbani lakini ananiambia atarudi lakini harudi

Wazazi wake ndio wanakataa arudi nyumbani nimebadilisha tabia yangu na nimeokoka, na nampenda mke wangu sana," Alieleza Alphonse.

Baada ya kumfikia mkewe, alisema kwamba ni kweli alikuwa anahanya na ndio maana alimuacha.

"Ndio alikuwa na wanawake wengi ndio maana nilitoka kwenye ndoa,lakini nitarudi anipe tu muda mfupi nitarudi."

Je Bi Jeska anastahili kumrudia mumewe au anapaswa kumchunga zaidi?