- Bwana Stephen alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe ambaye walikosana naye kwa ajili ya vitina kutoka kwa familia
Bwana Stephen alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe ambaye walikosana naye kwa ajili ya vitina kutoka kwa familia.
"Naomba nipatanishwe na mke wangu ambaye tulikosana naye kutokana na vitina kutoka kwa mashemeji na familia, ambao walisema kwamba nilikuwa naenda nje ya ndoa na kuniacha,"Stephen Alieleza.
Huku baada ya kumfikia mkewe alisema kuwa;
"Mimi nishaaolewa na nimekwambia uendelee na maisha yako, nikiwa naye alikuwa anaenda nje ya ndoa na kuniambia kwamba anaweza fanya ngono na mwanamke mwingine na kuniacha
Alinitesa katika ndoa, ambapo walinitusi wakisema kwamba siwezi pata ujauzito, na sasa nimepata, nikimwambia twende kwa daktari nilikuwa naenda pekeyangu alinifukuza na kuniambia nitoke niende kwamba kuna mwanamke mwingine anapaswa kuwa kwa nyumba yake
Alimpa mke wa bosi yake mimba, sijawahi muona mwanamume anamlilia mwanamke ilhali amemkataa uliniambia una wanawake wa kutosha
Huyu mwanamume niko naye akiniacha nitarudi kwako asipo niacha potea."