Patanisho: Jamaa atema mkewe baada ya kumpata na mipango tatu ya kando

Muhtasari

•Juma alisema walikosana na mkewe baada ya kukataa kulipa mkopo wa Sh13,000 ambao alikuwa anamdai licha ya kuwa walikuwa wamekubaliana angelipa.

•Alieleza kuwa alivutiwa na urembo wa mkewe licha ya kuwa amempiku kiumri na takriban miaka kum

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Donald Juma (25) alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Teresia Muthoni (35) ambaye walitengana kufuatia mzozo kuhusu pesa.

Juma alisema walikosana na mkewe baada ya kukataa kulipa mkopo wa Sh13,000 ambao alikuwa anamdai licha ya kuwa walikuwa wamekubaliana angelipa.

Alisema mzozo baina yao ulikuwa mkubwa kiasi cha kwamba waliwasilisha kesi kwa polisi na kwa chifu.

"Kuna pesa nilikuwa nimemkopesha. Ilifika mahali nikaitisha hiyo pesa ikawa hataki kulipa akaanza kusumbua kidogo. Mwenyewe alipigia polisi tukaenda mpaka kituoni. Alipohojiwa alikubali kwamba alikuwa na deni langu. Tulipofika kwa polisi nilimtusi askari kidogo nikamwambia hiyo ni ushenzi. Mkubwa alipokuja alikubali na akasema angekuwa ananilipa kila wiki shilingi elfu tatu. Alilipa miezi miwili ikafika shilingi elfu sita" Juma alisimulia.

Juma alisema baada ya miezi miwili walizozana tena na wakatengana kwa kipindi cha  miezi kadhaa kisha wakarudiana.

Alidai kwamba aliporejea aligundua kuwa mkewe alikuwa na mipango tatu ya kando, jambo ambalo lilifanya mahusiano yao kufikia kikomo.

"Tuliachana kidogo. Juzi tulirudiana ikafika mahali nikaenda ushago. Kurudi nikapata kumbe ako na watu tatu. Mpaka mwingine alikuwa anamkujia usiku na gari. Baada ya hapo aliniblock kila mahali. Tumechumbiana kwa kipindi cha mwaka mmoja" Alisema. 

Juhudi za kumpatanisha Juma na mkewe ziligonga mwamba kwani simu ya Muthoni ilikuwa imezimwa.

Baada ya hayo Juma alifichua kwamba lengo lake lilikuwa kuomba Muthoni msamaha tu wala sio kurudiana kwani tayari amepata mpenzi mwingine.

Juma alieleza kuwa alivutiwa na urembo wa mkewe licha ya kuwa amempiku kiumri na takriban miaka kumi.